Timu ya Taekondo kaunti ya Taita Taveta imepata ufadhili wa shilingi laki moja kuiwezesha kushiriki mashindano ya East and Central Africa (Chairman’s Cup) yatakayofanyika katika ukumbi wa KPA, Makande kaunti ya Mombasa kuanzia siku ya Jumamosi.

Waziri wa Vijana, Michezo, Jinsia, Tamaduni na Sanaa Bw. Bigvai Mwailemi ametaja spoti kama mojawapo wa fani zinazosaidia kukabiliana na changamoto za ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana pamoja na kudorora maadili kwa jamii hivyo kusistiza hoja ya kuweka mikakati ya kutosha kuboresha michezo.

Akiongea wakati wa kupeana fedha hizo, waziri Bigvai Mwailemi amesema licha ya changamoto zinazoendelea kushuhudiwa, vijana kama nguzo ya jamii wanastahili kutumia raslimali zilizopo kuboresha talanta zao ili kujikimu kimaisha.

“Tutatilia maanani michezo tukitambua kwamba hii huenda ikawa ajira kwenu. Wakilisheni kaunti hii kwa umakini na muandikishe matokeo bora. Kando na changamoto zilizopo kama za ukosefu wa vifaa, sisi kama serekali tutawashika mkono kwasababu gavana Granton Samboja amehakikisha michezo kaunti hii zinaimarika,” alisema.

Hatua ya waziri Mwailemi inajiri wakati ambao gavana Granton Samboja anasistiza hoja ya kuboresha sekta ya michezo. Kaunti itaangazia hii kuboreshwa kwa viwanja, kuanzishwa kwa kambi za michezo kama riadha, kandanda, voliboli na mengineyo.

Timu ya taekwondo kushiriki mashindano ya ‘Chairman’s’, pwani baada ya waziri kufadhili.

Leave a Reply